Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa baada ya balozi wa Tuzo za Sinema Zetu internationa Film Festival Elizabeth Michael 'Lulu' kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela hawajatafuta mbadala wake.

Mhando amejibu swali aliloulizwa wakati wa utangazaji wa vipengele vya tuzo za SZIFF zinazotarajiwa kufanyika April Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Akitolea ufafanuzi suala hilo,Mhando amesema kuwa mchakato wa kumpata balozi wa SZIFF kwa hiyo baada ya matatizo ya Lulu hawakuona umuhimu wa kupata mtu mwingine ,kwani muda haukuwa rafiki kwao.

"baada ya kutokea kwa matatizo kwa balozi wetu wa SZIFF Lulu, ambapo ili kumpata mwakilishi mwingine kunachukua muda mrefu hatukuona umuhimu wa kufanya hivyo na kuacha tuendelee na mchakato wa tuzo zetu ambazo tayari ulikua umeshaanza,"amesema Mhando.

Tuzo za SZIFF zilizinduliwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe ikiwa ni katika mchakato wa awali kabisa wa timu ya SZIFF kwenda mikoani kwa ajili ya kutafuta filamu mbalimbali huku balozi wa tuzo hizo Lulu akitambulishwa kwa mara ya kwanza kabisa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na aliyekuwa Balozi wa Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu (SZIFF) Bi. Elizabeth Michael alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa tuzo hizo Oktoba mwaka jana jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zinaratibiwa na Azam Media zinatarajiwa kutolewa  April Mosi ambapo zinazoshirikisha filamu za Kiswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...