*Awaambia wakazi wa Kanda ya Ziwa wafike kuona burudani, Msama awahakikishia usalama, maandalizi yamekamilika

Na Said Nwishehe,Globu ya jamii

MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za Injili John Lissu amewaomba mashabiki wa muziki huo na Watanzani kwa ujumla hasa wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 1 mwaka huu.

Lissu ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia Tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu litafanyika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza siku ya Aprili 1 na Aprili 2 litafanyika mkoani Simiyu katika uwanja vya Halmashauri mjini Bariadi.

Mwanamuziki huyo ameeleza kuwa wanamuziki mbalimbali maarufu wa muziki wa Injili ndani na nje ya Tanzania wataonesha vipaji vyao vya kuimba,hivyo kikubwa ni wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Tamasha hilo ambalo huwa linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion kupitia Mkurugenzi Mkuu Alex Msama ,wamehakikisha kuwa kutakuwa na  idadi kubwa ya wanamuziki wa Injili ili watu  wataofika kwenye tamasha hilo wapate burudani inayoambatana na ujumbe wenye kumpendeza Mungu

"Tunawaomba wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla tukutane uwanja vya CCM Kirumba siku ya Aprili 1 mwaka huu,wanamuziki wa Injili tumejiandaa vizuri,mashabiki karibuni muone kile ambacho tumekiandaa kwa ajili yenu.

" Siku hiyo mashabiki wa muziki wa Injili watarajie  mambo makubwa zaidi hasa kwa kuzingatia ukubwa wa Tamasha hilo nwa kwamba linafanyika wakati wa Pasaka na mwaka huu tupo Kanda ya Ziwa kwa mara ya kwanza,"amesema John Lissu.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. lex Msama kushoto  akifafanua kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu, mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar,kulia ni mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za Kiroho (injili) John Lissu akifurahi jambo kwenye mkutano huokuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. lex Msama kushoto  na Mwanamuziki wa Injili John Lissu wakiimba wimbo  wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kanda ya ziwa Aprili 1 na 2 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...