Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapindizi(UVCCM), Mkoa wa Kigoma wametakiwa kubuni miradi ya kimaendeleo kwa lengo la kupunguza kuomba misaada na kubwa zaidi kujiimarisha kwenye uchumi ili kuunga mkono kauli mbiu ya Uchumi wa viwanda.
Mwito huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa MNEC, Kilumbe Ngenda aliyekuwa mgeni rasmi, Katika Baraza la Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kigoma katika uchaguzi wa wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM Mkoa na kumthibitisha Katibu wa uhamasishaji na chipukizi.
Ambapo aliwataka vijana hao kubuni miradi na kuendeleza miradi waliyonayo kama jumuiya nyingine zinavyo fanya na kuwataka kuwa na miradi yao binafsi ili kupunguza tabia ya kutembea na mabakuli kuomba.

Pia ametoa cherehani tatu kwa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Mwandiga na kuwataka waendelee na jitihada za kuhakikisha vijana wote wanakuwa na shughuli za kufanya na kila Wilaya wabuni miradi."Sisi viongozi tutahakikisha tunawasaidia kuwawezesha ili kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wengi,"amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Wa Kigoma, Silvia Sigura amesema wao wamejipanga kufanya siasa za uchumi na si siasa za maneno na kwa kudhihirisha hilo wmeanza harambee kwa vijana katika baraza lililofanyika na kufanikiwa kuchangisha mifuko ya saruji 130 ili kuanza kujenga vibanda 12 katika kiwanja chao.
Amesema kwa michango walioipata watahakikisha wanaanzisha miradi kwa kila wilaya na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana ili wajiajiri katika masuala ya ujasiriamali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...