Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
MABWENI mawili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Moto huo ulianza kuunguza mabweni hayo saa tatu usiku na chanzo chake hakijajulikana.Hata hivyo inadaiwa huenda chanzo kikawa ni umeme ingawa bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa moto huo.
Akizungumza leo, kwa njia ya simu na Michuzi Blogu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ,Edward Bukombe amesema atatoa taarifa rasmi na kwa sasa yupo eneo la tukio hilo."Nipo eneo la tukio na baada ya hapo nitakupa taarifa rasmi."
Baadhi ya wanafunzi wote waliopatwa na mshituko wa tukio hilo wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya, ambapo inaelezwa walikuwa wanafunzi zaidi ya 15 waliopelekwa katika hospitali hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...