Na Mwamvua Mwinyi,Pwani.
JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata wahamiaji haramu kumi raia wa nchi ya Ethiopia ,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Jeshi hilo pia, limemtia nguvuni mwanamke -Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye silaha aina ya shortgun, huko kijiji cha Manda Mazingara kata ya Miono,tarafa ya Mkange wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP), Jonathan Shanna alisema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa machi 26, wakiwa porini ,Pingo Shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze na askari waliokuwa doria kufuatia kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Akielezea matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Tagen Alam (19), Abraham Wolde (19) na Musama Kamal (16).Wengine ni Abush Tamaskel (16), Ayela Erapo (18) na Ngusie Kechine (18), Zarabel Faisa (16), Tsedhj Yshgee (19), Teyey Ally (18) na Tuktigo Clemag (17).
Watuhumiwa wote hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.Kamanda Shanna alielezea ,jeshi hilo linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu waliowasaidia kuingia nchini bila kufuata utaratibu wa sheria.Katika tukio jingine , mwanamke aliyejulikana kwa jina la Felister Mtinga (30-36) amekutwa kitandani akiwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Moreto,iliyopo Chalinze.
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akizungumza kuhusiana na misako na doria zinazoendelea Mkoani humo.
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akiakionesha baadhi ya siraha alizokamata.
Wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia ambao wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani ,huko porini Pingo shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...