Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Jumapili Machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi 10 ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani akipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Inasemekana majeruhi waliopelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wengine wao wamekatika viongo mbalimbali vya mwili.Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya.Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ,aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini .
Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe.

"Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...