Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim pamoja na Balozi wa Taifa la Palestina nchini Tanzania Hazem Shabat wametia saini ya mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya afya.
Kupitia mkataba huo Taifa la Palestina pia litasaidia katika kuleta madaktari kwa ajili ya kutibu magonjwa yakiwamo ya uti wa mgongo ambapo madaktari wao na wa Tanzania watafanya kazi pamoja ya kutoa huduma za afya.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri Mwalim amesema kuwa wanatambua kuna changamoto katika kutibu baadhi ya magonjwa nchini, hivyo madaktari bingwa wa Palestina na madaktari bingwa waliopo nchini watatumia fursa ya mkataba huo wa ushirikiano katika kutoa huduma za tiba kwa Watanzania.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano,chini ya Rais, Dk.John Magufuli imekuwa na jitihada  mbalimbali za kuboresha sekta ya afya lakini mkataba uliotiwa saini leo unatoa fursa ya kuimairisha pia utoaji wa chanjo na dawa.
Amesema mkataba huo umejikita kwenye maeneo mbalimbali na baadhi ni kusaidia katika kutoa huduma za afya, kusaidia upatikanaji wa dawa, kuimarisha eneo la Tehama ili kuboresha huduma hasa kwa kuzingatia teknolojia ya habari na mawasiliano itasaidia kuimarisha mfumo wa kutunza kumbukumbu za sekta ya afya.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakibadilishana mikataba na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania baada ya kutiliana saini kwa ajili ya  ushirikiano kati ya Tanzania na Palestina katika sekta ya afya, Hafla ya kutiliana saini imefanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakizungumza na mara baada ya kusaiini mikataba ya ushirikiano katika sekta ya Afya  kati ya Tanzania na Palestina kushoto ni Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania.
 Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo, Kulia ni Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.
Baadhi ya maofiza kutoka wizaya ya Afya wakiwa katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...