Na Said Mwishehe, Blog ya jamii
AZAKI tano kwenye Kamati ya Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na
uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini
Tanzania(TEITI) zimpongeza Ripoti ya Nane ya taasisi huku
wakishauri fedha zinazopatikana kwenye madini zitumike kwa
manufaa ya kizazi cha sasa na kesho.
Kwa mujibu wa Azaki hizo zisizo za kiserikali ambazo ni Publish What You Pay(PWYP-TZ), Gender and Disability , Interfaith base, Trade Union na Corventional NGO,s ambazo si za kiserikali
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ripoti hiyo ambayo imezinduliwa rasmi na Waziri wa Madini Angella Kairuki, Mjumbe wa TEITI kutoka Azaki hizo za kiraia anayewakilisha Taasisi za kidini, Grace Masalakurangwa amesema baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hiyo ni vema ikafikishwa kwa umma.
Ambapo wamefafanua ni vema pia ripoti hiyo ikawekwa kwenye lugha rahisi na nyepesi kueleweka na kwa kufanya hivyo itasaidia watu wengi zaidi na wa makundi mbalimbali kuichambua.
"Tumewaita waandishi wa habari kwa lengo la kuwaelezea namna ambavyo tumefurahishwa na kupongeza ripoti ya TEITI ambayo imezinduliwa leo. Ombi letu kwao ni vema ripoti hiyo ikawekwa kwenye lugha rahisi ili iweze kuchambuliwa," amesema Masalakurangwa kwa niaba ya azaki hizo ambazo zimesisitiza uzinduzi ni jambo moja na wananchi kutoa maoni yao ni hatua nyingine.
Pia ametoa ombi sasa umefika wakati wa Serikali kutunga kanuni kuhusu sekta ya madini ingawa wanatambua sheria ya madini ya mwaka 2015 ipo lakini wanaamini kukiwa na kanuni kutasaidia kwani sheria hiyo inazungumza kwa upana zaidi.
Akifafanua kuhusu fedha ambazo zinapatikana kwenye eneo la madini, mafuta na gesi asilia ni vema Serikali ikahakikisha zinatumika katika kufanya mambo yenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho na kueleza wao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya TEITI lakini wanayo nafasi ya kuchambua na kutoa maoni yao kuhusu ripoti ambayo imezinduliwa.

Mjumbe wa TEIT kutoka Asasi za Kiraia anayewakilisha Taasisi za Kidini, Grace Masalakurangwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti iliyozinduliwa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe kutoka PWYP-TZ, Petro Ahham akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwajibikaji wa serikali kwenye rasilimali za Tanzania ili kuwanufaisha wazawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...