
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo mjini Dodoma,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka,Alex Msama amesema sasa ni zamu ya kanda ya kati Dodoma,ambapo leo tamasha hilo linafanyika.

"Tunamshukuru Mungu tumefanikisha salama tamasha la pasaka kanda ya ziwa,kwa maana kwamba ya mkoa wa Mwanza na Simiyu,kesho tunahitimisha kanda ya kati Dodoma,ndani ya uwanja wa Jamhuri'',alisema Msama.
Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo ndani ya mkoa wa Dodoma,yamekwishakamilika na kwamba kila kitu kiko sawa,alisema na kuongeza kuwa hata waimbaji wameishawasili tayari kwa kumtukuza Mungu kupitia nyimbo zao za injili.
Amesema tamasha hilo litakuwa la tofauti,kwa sababu waimbaji wengi ambao hawakuwepo Mwanza na simiyu,watapata nafasi ya kuonekana na kuimba mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma,watakaofika kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika kesho April 8 2018,ndani ya uwanja Jamhuri
Msama amewawataja baadhi ya waimbaji baadhi ya Waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo ni Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya ambaye tayari amekwishawasili mjini Dodoma,Rose Muhando ambae ataendeleza uzinduzi wa albam yake mpya ya “Usife Moyo” huku akitamba na kibao chake kilichomo kwenye albam hiyo kijuliakano kwa jina “Lazima Wakae” .
Msama anawakaribisha wakazi wa mji wa Dodoma na vitongpoji vyake kujitokeza kwa wingi leo ili kushuhudia burudani ya muziki wa injili huku wakipata uponyaji na wokovu kwa njia ya uimbaji kwa kiingilio cha shilingi elfu 3000/= tu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...