Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliosaidia ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na viongozi wengine pamoja na wadau waliosaidia ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia jijini Arusha kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya familia za askari polisi baada ya kufungua rasmi nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la askari polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Gari maalumu la kunyunyizia maji ya kuwashawasha likionesha namna kikosi cha kutuliza ghasia cha Jeshi la Polisi kinavyoweza kupambana na waandamanaji katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018. Aprili 7, 2018.
Askari wa Jeshi la Polisi wa kikosi maalumu cha kulinda viongozi wakionesha namna kinavyoweza kupambana na maadui katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo Aprili 7, 2018
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...