Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru na kuipongeza Taasisi ya Kiraia ya Zanzibar Relief and Development Foundation { ZANRDEF} kwa uamuzi wake wa kusaidia huduma za msingi ya Kijamii za Maji safi katika azma yake ya kuona maisha ya Wananchi yanaendelea kustawika.
Alisema uamuzi huo wa ZANRDEF utasaidia kuwapunguzia machungu Wananchi walio wengi kupata huduma hizo sambamba na kuiunga Mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mipango yake ya kuwasogezea karibu mahitaji ya msingi Wananchi wake.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa shukrani hizo wakati akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Mahonda mara baada ya kukikagua Kisima cha Maji safi na salama kinachochimbwa katika Skuli ya Mahonda kwa msaada wa Taasisi ya ZANRDEF.
Alisema zipo changamoto nyingi za upatikanaji wa huduma za Maji safi na salama kwa Wananchi walio wengi Visiwani Zanzibar licha ya juhudi kubwa inayoendelea kuchukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na washirika wa Maendeleo kuitafutia ufumbuzi changamoto hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifika Skuli
ya Mahonda kukagua uchimbaji Kisima cha Maji safi na salama
kitakachowaondoshea usumbufu Wanafunzi na Walimu wa Skuli hiyo.
Balozi Seif pamoja na Uongozi wa Wilaya ya Kaskazini B na Kamati ya
Maendeleo ya Jimbo la Mahonda wakishuhudia harakati za Uchimbwaji wa
Kisima cha Maji safi na Salama katika Skuli ya Mahonda Msingi na
Sekondari chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Taasisi hiyo Bwana Doto
Saleh wa kwanza Kulia aliyevaa Kofia ya Manjano.
Balozi
Seif Kati Kati akipongeza na Kuishukuru Taasisi ya Kiraia kwa uamuzi
wake wa kusaidia huduma za Maji Safi na Salama Ndani ya Skuli ya Msingi
na Sekondari ya Mahonda. Kushoto
ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Nd. Rajab Ali Rajab na
Kulia yake ni Katibu wa ZANRDEF Bwana Ali Mohamed Haji.
Harakti za uchimbwaji wa Kisima cha Maji safi na Salama katika Skuli ya
Mahonda zikiendelea licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha muda mrefu.
Mkuu
wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Rajab Ali Rajab akitoa shukrani kwa
Uongozi wa Jimbo la Mahonda na Taasisi ya Kiraia ya ZANRDEF kwa jitihada
za kusogeza huduma za Maji safi katika Skuli ya Mahonda Msingi na
Sekondari. Picha na – OMPR – ZNZ.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...