Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekabidhi shilingi milioni 5 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa alipotembelea ujenzi wa kituo hicho cha polisi tarehe 13.11.2017 na wananchi kumuomba kuchangia ambapo ukamilifu wa kituo hicho utasaidia kuhudumia kata 13 zilizopo katika bonde la ziwa Rukwa.



Sambamba na hilo Mh. Wangabo pia aliwasilisha ahadi ya Milioni 10 aliyoitoa Mkuu wa jeshi la Polosi nchini IGP Simmon Siro alipotemblea Mkoa wa Rukwa na kuongeza kuwa kuna shilingi milioni 1.5 ambayo pia ni ahadi ya mkazi wa bonde la ziwa Rukwa anayeishi nje ya Mkoa ambaye hakuhitaji kutajwa jina lake.

“Nimekuja kutekeleza ahadi yangu ambayo inaendana na mlichonisomea, mlisema ili kituo cha polisi kikamilike mlihitaji shilingi milioni 4, mkaniomba niwatafutie, mimi nimekuja na shilingi milioni 5, ila nilituma timu yangu ili kuangalia ile gharama kama ilikuwa sahihi, nikaambiwa na hiyo timu kuwa inahitajika shilingi Milioni 22, alipokuja Kamanda IGP niliteta nae na alipoona umuhimu wa kituo hiki aliahidi shilingi Milioni 10,” Mh. Wangabo alisema.

Wakati akikabidhi fedha hizo kwenye mkutano na wananchi niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya alimtaka Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Hamis Mongela kukiri kupokea fedha hizo huku ahadi nyingine zikiendelea kufuatiliwa ili ujenzi wa kituo hicho ukamilike kwa wakati, nae Hamisi alikiri kupokea fedha hizo.

Diwani wa kata ya Mtowisa Mh. Edgar Malinyi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni juhudi za wananchi wanaotaka usalama wa vitu na mali zao wakishirikiana na polisi huku mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa akisesama kuwa wananchi hawatakata tamaa hadi kituo hicho kikamilike kwani ujezi wake ulianza tangu mwaka 2002.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...