Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy (wa tatu kushoto,) akikabidhi vifaa vya kusaidia upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa (wa pili kushoto), katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wengine ni watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy(kulia), akikabidhi kadi ya bima ya afya (NHIF) kwa mmoja wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi , Joy Jacob katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto (mstari wa nyuma) ni kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa, watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Baadhi ya watoto 200 waliopewa msaada wa kadi za bima ya afya (NHIF) na benki ya Barclays Tanzania wakionyesha kadi zao katika hafla hiyo katika hafla ambayo benki hiyo pia ilidhamini kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...