Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank Tanzania, Selemani Ponda akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matokeo ya benki ya mwaka 2017. Kushoto kwake ni Kaimu Afisa wa operation David Lusala na Kulia ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Issa Hamisi.

BENKI ya Exim imeendelea kubaki katika nafasi ya tano kwa ukubwa ikiwa na rasilimali zenye thamani ya shilingi trilioni 1.6 zitokanazo na ukuaji wa amana kutoka kwa wateja.

Ikiwa ni Benki ya kwanza nchini kufungua Benki tanzu nje ya nchi, Benki ya Exim imeendela kufanya vizuri pia huko ughaibuni. Benki tanzu ya Jibuti ni ya nne kwa ukubwa nchini humo wakati ile ya Komoro ni ya pili visiwani humo. Jibuti ilipata faida ya shillingi billioni 6.5 wakati Komoro walipata faida ya shilingi bilioni 4.8.  Marejesho ya mtaji kwa benki hizo yamekuwa juu zaidi ya kiwango kilichotarajiwa kwa asilimia 50 na 40 kwa Jibuti na Komoro.

Nchini Uganda, ambapo kuna Benki tanzu pia, Benki imeendelea kufanya vizuri na kupunguaza kiwango cha hasara. “Ni mataraji yetu kuwa Uganda itafuata nyayo za Jubuti na Komoro, hivyo kuanza kutengeneza faida kubwa mwaka 2018”, alisema Kaimu Mkurugenzi mkuu, Bwana Selemani Ponda.

Katika mahesabu ya mwaka 2017, faida jumla itokanayo na shughuli za kibiashara nchini Tanzania ziliathirika kidogo kutokana na  mikopo mibaya na pia taratibu mpya za kiuhasibu lenye kuhitaji tengo zaidi kwenye mikopo mibaya. Hata hivyo, matokeo ya kifedha ya biashara mbalimbali katika utendaji nchini Tanzania ukiondoa kuharibika kwa mikopo, Benki imeweza kupata faida ghafi  ya shilingi bilioni 39 kutokana na ongezeko la tengo kwenye mikopo mibaya faida ilishuka mpaka shilingi bilioni 9.6.

“Benki imejivunia kuwa na benki tanzu nje ya nchi, hivyo kuwa na wigo mpana wa kutengeneza faida kutokana na hali nzuri ya uchumi katika nchi husika”, aliongeza kaimu mkurugenzi mkuu, bwana Selemani Ponda.

Exim itafuta mikopo yenye mingine zaidi robo ya kwanza ya mwaka 2018 kufuatana na taratibu mpya za kibenki na kufanya uwiano wa mikopo mibaya kuboreka kutoka asilimia 14.63 mpaka asilimia 8.95. Kaimu mkurugenzi mtendaji bwana Selemani Ponda amethibitisha jitihada za Benki za kuendelea kuboresha ubora wa mikopo kwa lengo la kufikia uwiano wa chini ya asimlimia 5% mpaka mwisho wa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...