Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE Wajasiriamali wametakiwa kujiunga na Jukwaa la Wanawake ili kujiinua kiuchumi.
Mwito huo umetolewa na Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati akizindua kikundi cha wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana.
Katika hatua nyingine Kalekezi amewataka wanawake hao kuacha unafiki na kupendana jambo litakalowasaidia kusonga mbele kwenye umoja wao huo.
Alisema Dunia imeanzisha Jukwaa la Wanawake ambapo wanawake watakuwa wakukutana kujadili changamoto walizo nazo na jinsi ya kuzikabili pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za maendeleo."Jukwaa ili na sisi linatuhusu hivyo hatuna budi kujiunga nalo kwani huko tutapata wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali pamoja na biashara hivyo ni vizuri tukalichangamkia" alisema Kalekezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG) Jane Magigita alisema wakati huu si wakulala bali ni wakuangalia fursa nyingine ili kujikomboa kiuchumi.Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kupambana vilivyo ili kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi.
Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, Juliana Richard, Mwenyekiti, Anjela Mwamakula na aliyevaa miwani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
Wanachama wa Kikundi cha Mshikamano Mchikichini Sokoni wakiwa kwenye uzinduzi wa kikundi chao.
Hapa wakiserebuka.
Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...