Na Yusuph Mussa, Tanga
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongo (NCAA) imedhamini mashindano ya Ngorongoro Marathon kama sehemu ya njia ya kukuza utalii kwenye eneo hilo lenye vivutio vya pekee duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Aprili 11) jijini Tanga, Naibu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu, alisema mashindano hayo yatakuwa na faida kubwa kwenye nyanja za utalii na kuwezesha watu wengi ndani na nje ya nchi kuvutiwa na hifadhi hiyo.
"Tumeamua kudhamini mashindano haya ya Ngorongoro Marathon yanayofanyika Aprili 21, mwaka huu. Nia ya kudhamini mashindano haya, kwanza ni kufanikisha mashindano yenyewe na pili ni kuweza kutangaza utalii wetu.
"Tunaamini sisi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tuna dhima kubwa kuona watalii wa ndani na nje wanaongezeka. Lakini ili waongezeke ni lazima tutumie njia mbalimbali za kutangaza vivutio vya Hifadhi za Ngorongoro ambavyo ni vya kipekee duniani" alisema Bangu.
Bangu alisema Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, pia imekuwa na changamoto ya ujangili na uvamizi, hivyo kwa kutumia mashindano hayo, watawaeleza wananchi wajue umuhimu wa hifadhi hizo kwa maslahi ya nchi.
Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).
Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa)

Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).

Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...