Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro amefungua na kuongoza mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga uliolenga kujadili namna ya kufanikisha zoezi la chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoani humo. 

Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Aprili 17,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

Akifungua mkutano huo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo imeanzisha chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.

Matiro alisema saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza nchini Tanzania kwa kusababisha vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ambazo zote zinasababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akina mama vitokanavyo na saratani hivyo kunahitajika juhudi na ushirikiano zaidi kupunguza vifo hivyo.

“Lengo la kuanzisha chanjo hii ni kukinga mabinti kutokana na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake,na walengwa wa chanjo hii mwaka huu ni wasichana wote wanaotimiza miaka 14 ambapo katika mkoa wa Shinyanga wasichana wasiopungua 29,479 watachanjwa”,aliongeza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga 
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga. 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...