Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TAASISI ya Tulia Trust imezindua Tulia Marathon itakayofanyika Mei 6 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Tulia Marathon, Mratibu wa Mashindano hayo na Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson amesema fedha ambazo zitapatikana kwenye mashindano zitatumika katika afya na hasa afya ya mtoto kwa jamii ya Mbeya.

Dk. Tulia amesema amekuwa anaungwa mkono na wadhamini katika kufanikisha taasisi hiyo kuendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali katika kuandaa michezo.

Amefafanua mashindano ya mbio hizo yatakuwa na muonekano tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika nchini kwani yamejumuisha kila kundi katika jamii.

Aidha ameongeza mashindano hayo yatakuwa ya kilomita  42 Full  , Half  Marathon 21 , wanafunzi kwa mbio za kilomita Tano , mbio za baiskeli kilomita 150 kwa wanaume na kilomita 75 kwa wanawake, kilomita tano watakimbia watu kwa ajili ya kujifurahisga  na watoto watakimbia kilomota mbili.

Amesema fomu za maombi kwa watakaoshiriki mashindano ya Tulia Marathon zinapatikana katika tovuti ya www.tuliatrust.org

Wadhamini wa mashindano ya Tulia Marathon hayo ni Mo Dewj Foundation, Mantra Tanzania, Tatu Muzuka pamoja na Derm Electrics T LTD.
01.Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa Tulia Marathon itakayofanyika Mbeya, leo jijini Dar es Salaam.
02. Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga akizungumza kuhusiana na kudhamini mashindano ya Tulia Marathon
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akimkabidhi tshirt, Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga kwa kutambua mchango wa Tatu Muzuka katika kudhamini mashindano hayo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...