Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imekosa mashine ya X-RAY ,hali inayosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila.

Akizungumza na Michuzi blog, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ameeleza ujenzi wa hospitali ya Mkamba unaendelea vizuri hadi sasa nyumba ya mganga, chumba cha upasuaji, maabara na wodi ya wazazi zipo katika hatua nzuri na hii ni kwa msaada wa serikali.

Mwandambo ameeleza wanapokea akina zaidi ya 300 kwa ajili ya kujifungua, hivyo ujenzi wa hospitali ya Mkamba utapunguza adha hiyo.Aidha meeleza kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa mashine ya X-RAY tangu ilipoanzishwa na bado wanapambana na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ili kutatua changamoto hiyo.

Pia amefafanua kuwa rufaa za kokosa damu zimepungua kutoka asilimia 28 hadi asilimia 3 na bado wanaendelea kuelimisha wananchi kuhusu kulima na kula mboga za majani sambamba na matumizi ya dawa za kuongeza damu kwa wajawazito.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde ameeleza madaktari wapo ila hawana mashine ya X-RAY hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa hospitali nyingine.

Aidha Munde amesema madaktari wapo na chumba cha X-RAY kipo tayari kwa kutegemea mashine kutoka kwa Wizara husika lakini bado ni kitendawili.Pia Munde ameongeza mwaka jana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Ulega walikuwa na maongezi na aliyekuwa Balozi wa China nchini kuhusu kupatikana kwa mashine hiyo.

"Na maongezi hayo yana matumaini kidogo baada ya kufika muafaka wa balozi huyo kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo,"amesema.Amefafanua kama Halmashauri wanatakiwa kuchangia dola za Marekani 40,000 ambazo zinatakiwa zilipwe kwa wasambazaji ndipo dola 30,000 zitolewa na balozi wa China kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo.
 Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti  wa Afya  wa kituo cha Mkamba,Haji Abdallah Pepo mara baada ya kukagua mradi wa majengo ya Kituo cha Afya Mkamba,Mradi huo umefikia hatua ya mwisho za ujenzi wa miundombinu ambapo ujenzi huo umeelekezwa kwenye chumba cha upasuaji,wodi ya wazazi,Maabara na Nyumba ya Mganga.

 Muonekano wa majengo ya kituo cha Afya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Hosptal ya Wilaya kukosa mashine ya X-RAY,hali inayosabaisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Mhimbili na Mloganzila.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kukosekana kwa huduma ya mashine ya X-RAY ,hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa katika hospitali nyingine.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...