Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma (75)amefikishwa katika Mahakama ya Durban  nchini South Afrika kujibu tuhuma za rushwa zinazomkabili ikiwemo mpango wa ununuzi wa silaha uliogharimu mabilioni ya fedha ikiwa ni wiki saba tangu kiongozi huyo ajiuzulu.

Zuma amefikishwa mahakamani leo ambapo anashtakiwa kwa makosa 16 ya rushwa.Pia anashtakiwa kwa tuhuma za kupokea malipo 783 ambayo yanatia mashaka.

Hata hivyo baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo Zuma amekataa makosa yote hayo na kesi imehairishwa hadi Juni 8 mwaka huu.Wakati wa kesi hiyo maelfu ya wafuasi wake wamejitokeza kumuunga mkono Zuma wakiwa wamevaa fulana za picha na maelezo yanayoashiria kiongozi huyo aachiwe huru.

Hali hiyo ilimfanya Zuma licha ya kuwapo mahakamani hapo ilimfanya kuwa mwenye furaha na kuonesha kutabasamu kama ishara ya kutambua uwepo wao.Zuma (75) alijiuzulu February 14 kwa kushinikizwa na chama chake mwenyewe cha African National Congress (ANC) ambacho ni chama tawala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...