Total ambayo ni moja ya makampuni ya mafuta yanayoongoza nchini, imezindua huduma mpya na maalumu ya kuosha magari ijulikanayo kama “Total Wash” ambayo kwa sasa inapatikana katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mauzo wa Total Tanzania, Nikesh Mehta alisema huduma hiyo mpya ina lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwani wateja wataoshewa magari yao kwa haraka zaidi kwa kupitia utaalamu wa ‘jet wash.

“Tunalo lengo pia la kuhakikisha kuwa huduma zote zinapatikana katika kituo kimoja hasa kwa wateja wa Total ambao hawana muda mrefu wa kusubiri tutahakikisha wanapata huduma iliyo bora baada ya kujaza mafuta na kupata huduma nyingine za kiufundi tunazotoa,” alisema.

Alisema huduma hiyo imepokewa vizuri na wateja katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access.

“Kuna sehemu nyingi za kuosha magari lakini huduma hii ni ya kipekee kutokana na utaalamu na teknolojia inayotumika ambayo itahakikisha wateja wa Total wanapata huduma iliyo bora na ya viwango vya juu,” alisema na kuwataka wateja wengi zaidi wajaribu huduma hiyo.

Alisema kwa wateja wanaohitaji kutumia huduma hiyo, wanatakiwa kununua sarafu maalumu (token) katika maduka ya Total (Café Bonjour) yanayopatikana katika vituo vyao na kila sarafu itakuwa na kipimo cha muda kulingana na huduma inayotolewa..

Bw. Mehta alisema wana mpango wa kuanzisha huduma hiyo katika vituo zaidi nchini katika siku za hivi karibuni.

Total ina vituo 90 nchi nzima na inajivunia kwa kuuza mafuta na vilainishi vyenye ubora wa hali ya juu kama vile Total Quartz, Total Rubia na Special 4T lakini pia inajivunia kutoa huduma zinazoaminika na kukubalika kote.
Mmoja wa wahudumu wa Total akiosha moja ya magari kwa kutumia teknolojia mpya ya 'jet wash'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...