Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kufuatia Yanga kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika ratiba ya ligi kuu iko mbioni kupanguliwa.

Hilo linakuja baada ya Shirikisho la Soka Afrika CAF kupanga ratiba ya makundi mwishoni mwa wiki hii na kuonyesha tarehe za michezo itakayochezwa kwa kila kundi.

Yanga iliyopangwa kundi D akiwa na timu za Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria mechi zao wa kwanza zinatarajiwa kuanza Mei 6 mwaka huu.

Wawakilishi hao wa Tanzania na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom wataanza mchezo wao wa kwanza ugenini dhidi ya USM Alger Mei 6 na kisha baadae kuja kumenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.

Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.

Baada ya Ratiba hiyo ya mchezo wa kwanza wa Yanga wa Mei 6,  Bodi ya ligi haitakuwa na budi kufanya mabadiliko ya ratiba ya mchezo wa Yanga dhidi ya Mbao uliokuwa ufanyike Mei 5 na ule wa Mtibwa ambapo awali ulifanyiwa mabadiliko na kupangwa kucheza Mei 9 mkoani Morogoro.

Mei 12 Yanga ilipangwa kumenyana na Mwadui Mkoani Shinyanga na dhidi ya Prisons ni Mei 16 mkoani Mbeya.Mbali na mechi hizo Mei 20 ni Yanga dhidi ya Ruvu Shooting na wakimalizana na Azam mei 26.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...