MAFUNDI mitambo wa redio kutoka mikoa mbalimbali nchini wametembelea Shirika la Utangzaji Tanzania(TBC)kwa lengo la kupata mafunzo zaidi ili kuendelea kuboresha majukum yao kwa ufasaha.
Wakiwa TBC mafundi mitambo hao wamepata nafasi ya kutembelea vitengo mbalimbali ambavyo vinahusika na masuala ya utangazaji katika shirika hilo.
Mafundi mitambo hao wametembelea TBS jana jijini Dar es Salaam na hatua hiyo ni muendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), ambalo limeamua kuwapiga msasa mafundi mitambo kutoka redio 25 za kijamii Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa mujibu wa Unesco ni kwamba mafundi mitambo hao licha ya kuata mafunzo kwa kukaa darasani, watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kwenda kwao TBS ni sehemu ya kuendelea kuwajengea uwezo. Mafunzo ambayo ni sa siku saba yanatarajia kumalizika Aprili 25 mwaka huu.
Principle
Engener kutoka TBC, Noel Mtenga akitoa ufafanuzi kuhusu gari la
kurushia matangazo la TBC 1 linavyofanya kazi wakati wa mafunzo kwa
vitendo kwa mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara
na Zanzibar.
Mwahariri
wa Habari za Kimataifa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),
Nyambona Masamba akiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii kuhusu
namna wanavyopata habari za Kimataifa pamoja na jinsi wanavyozihariri
kabla ya kurushwa hewani wakati wa ziara ya mafunzo yaliyofanyika katika
Shirika la Utangazaji(TBC).
Mtangazaji
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ramadhan Mpenda akiwaelezea
kiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii namna wanavyorusha habari
kwenye moja ya studio ya TBC 1 iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Fundi
mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Fanuel Elia akitoa
ufafanuzi kuhusu namna wanavoweza kupangilia vipindi kwenye chumba cha
kusimamia matangazo ya TBC 1 wakati wa ziara ya mafunzo kwa mafundi
mitambo wa Radio za jamii.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...