Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambapo anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano huo ambao Kaulimbiu yake ni “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja” unafanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa Theresa May na umefunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza.

Majadiliano ya Mkutano wa CHOGM 2018 yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi; na mustakabali wenye usawa zaidi.

Mijadala katika maeneo hayo ya kipaumbele itahusisha masuala mbalimbali ikiwemo, kukuza zaidi biashara na uwekezaji baina ya nchi za Jumuiya ya Madola kwa manufaa ya nchi wanachama na Jumuiya nzima; kukuza na kuendeleza misingi ya demokrasia; ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu pamoja na masuala ya uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi, uhalifu wa kimtandao na usafirishaji wa binadamu. 

Jumuiya ya Madola ilianzishwa mwaka 1949 kupitia Tamko la London ambalo lilikuwa ni matokeo ya Mkutano wa Mawaziri Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola.  Jumuiya ya Madola ina wanachama 53 ambapo kati ya hizo, nchi 19 ni za Afrika, 7 ni kutoka Asia, 13 ni kutoka nchi za Carribean na Mabara ya Amerika, 11 ni kutoka eneo la Pacific na nchi 3 ni kutoka Ulaya. 
Makamu wa Rais pia alishahudhuria mikutano mbali mbali inayoambatana na mkutano huo ukiwemo mkutano wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi pamoja na Mkutano wa Kutokomeza Malaria kabisa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikizungumza kwenye Mkutano wa  Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola wamekutana jijini London, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye Mkutano wa  Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola wamekutana jijini London, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola Wanakutana jijini London kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola Wanakutana jijini London kushoto ni Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...