MKUU  wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewatahadharisha wanaume wanaodhani wanaweza kukaidi wito wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.

Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano ya kipindi cha tathimini ya mchakato wa kudai haki za watoto waliotelekezwa ambapo amesema tangu Jumatatu zaidi ya 17,000 walifika ofisini kwake na Kati ya hao 4,400 wamesikilizwa. 

Aidha Makonda amesema kinachomfariji ni kuona idadi kubwa ya kinababa wanaofika ofisini kwake wanakubali kumlea mtoto ambapo hadi sasa familia 295 zimekubali kuhudumia mtoto na familia 29 zimepima DNA.* 

Hata hivyo  Makonda amesema baada ya zoezi hilo ataunda tume ya kuangalia changamoto zilizopo katika sheria ya matunzo ya mtoto* kisha kuifikisha kwa waziri husika kwaajili ya kufikishwa Bungeni kwaajili kufanyiwa marekebisho. 

Pamoja na hayo Makonda amesema hatoyumbishwa na baadhi ya watu wasiojua uchungu wanaopata kinamama kwa kubeza zoezi hilo kwakuwa yeye ametambua Mateso waliyokuwa wakipata kinamama waliotelekezwa. 

Makonda amesema ikitokea mwanamke aliefika ofisini kwake na kumshitaki mwanaume aliezaanae kisha uchunguzi ukafanyika na kubaini udanganyifu mwanaume anayo haki ya kufungua kesi ya kudhalilishwa na afisa ustawi wa jamii wa mkoa atalazimika kuwa shahidi mahakamani. 

WATU WENYE DHAMBI WANAPENDA GIZA NDIO MAANA UKIWASHA NURU WANAIBUKA KUPINGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...