KAMPUNI ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) imekabidhi magari 15 kwa wizara ya maliasili na Utalii kwa ajili ya kusaidia kulinda rasilimali ya wanyamapori nchini.

Magari hayo aina ya Toyota Landcruiser yalikabidhiwa jana kwa Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina,katika ofisi za Wizara ya Maliasili, jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi magari hayo yenye thamani ya Zaidi ya sh. Bilioni 1.5, Mkurugenzi msaidizi wa OBC, Molloimet Yohana, alisema kuwa msaada huo ni mahususi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili na ulinzi wa wanyamapori.

“Huu ni mwendelezo wa azma ya serikali ya UAE na OBC katika kuunga mkono mapambano hayo kwani tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara,”alisema.Alisema ushiriki wao katika uhifadhi wanyamapori utaendelea kwani ni mpango endelevu na kamwe hawatasita kusaidia pale itakapobidi.Akipokea msaada huo, Mwina alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa OBC ambao imekuwa ikitoa katika sekta hiyo,na kuwataka kuendeleza mahusiano na kutokatishwa tamaa na maneno yanayozungumzwa juu ya kampuni hiyo.
Magari 15 yaliyokabidhiwa na Kampuni ya OBC ya Loliondo.
Mkurugenzi idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 15 aina ya Toyota Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion 1.5 yaliyotolewa na kampuni ya uwindaji ya OBC,ya Loliondo kwa ajili ya shughuli za kuzuia ujangili na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji Dar es Salaam.
Mkurugenzi idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina akijaribu kuendesha moja ya magari 15 aina ya Toyota Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion 1.5 yaliyokabidhiwa na kampuni ya uwindaji OBC,ya Loliondo kwa ajili ya shughuli za kuzuia ujangili na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...