KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imepanga kutumia vyema mageuzi yanayoendelea katika sekta ya anga nchini kwa kuboresha zaidi huduma zake ili ziandane na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza, kwasasa kampuni hiyo inaandaa mikakati itayoiwezesha kujitanua ili kunufaika zaidi na ongezeko la idadi ya ndege za kitaifa na kimataifa linalotarajiwa kufuatia mageuzi hayo.

“Tunachokifanya Puma Energy ni kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya anga’’ alisema Tungaraza katika mahojiano yake na waandishi wa habari hivi karibuni katika Mkutano wa wadau wa sekta ya anga barani Afrika ulioandaliwa na Umoja Wa Mashirika ya Ndege barani Afrika (AFRAA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege nchini (ATCl) uliofanyika visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Alitolea mfano wa maboresho yaliyofanywa na kampuni hiyo katika mfumo wake wa huduma ya mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuwezesha kampuni hiyo kukidhi mahitaji ya usambazaji wa nishati hiyo ambayo yanayotarajiwa kuongezeka mara tu baada ya kukamilika kwa upanuzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three).

Alisema lengo la kampuni hiyo katika sekta ya anga ni kutoa huduma ya mafuta kwa bei ya ushindani kwa wateja wake huku pia ikizingatia kutoa huduma hizo kwa kukidhi mahitaji ya viwango usalama na ubora wa kimataifa.

"Linapokuja suala la usambazi wa mafuta ya ndege huwa tunajitahidi sana kuhakikisha tunawapa urahisi zaidi wateja wetu kwa kuhakikisha tunaratibu kila kitu sisi kuanzia uagizaji, utunzaji, uhifadhi na usafiri hadi kwenye vituo vyetu vilivyopo kwenye viwanja vya ndege kwa kutumia rasilimali watu wenye weledi zaidi katika suala hilo,’’ .

“Ni wazi tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’ alitaja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...