Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Jodhpur nchini India imemhukumu muigizaji wa filamu za kihindi Salman Khan (52) kwenda jela miaka mitano kwa kukutwa na tuhuma za ujangili.
Khan anadaiwa kwamba mnamo mwaka 1998 Khan akiwa katika maandalizi ya kutengeneza filamu yake ya Hum Saath Hain aliua swala wawili adimu kupatikana nchini humo maarufu kama Blackbucks huko Rajasthan India.
Akiongea nje ya mahakama wakili wa Khan Bw. Bhawan Sigh ameeleza kuwa mteja wake anaweza kukata rufaa na akikubaliwa anaweza kulipa faini au kuachiwa huru aidha hadi sasa Khan bado amewekwa gerezani kwa muda.
Bhawan ameeleza kuwa Khan alikamatwa akiwa na waigizaji wengine maarufu ambao ni Saif Ali Khan, Sonali Bendre, Tabu na Neelam Kothari ambao waliachiwa huru baadaye.
Abdul Rashid Salim Salman khan maarufu kama Salman Khan alizaliwa Desemba 23 1967, ni muigizaji, muongozaji wa filamu na mwimbaji ambaye amepata tuzo mbalimbali kama National film awards na Filmfare Awards. Khan amecheza filamu zaidi ya 90 zikiwemo Kuch Kuch Hota Hai (1998)
Hum Aapke Hain Koon (1994) na Ile ya kivita ya Karan Arjun (1995).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...