Na Humphrey Shao, GLobu ya Jamii

KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) ambayo ni moja kati ya wanafamilia AB InBev imeandaa shindano linalowahusisha matumizi ya ubunifu na teknolojia kwa wakulima.

Shindano hilo lililozinduliwa jana, litafikia tamati Mei 10 mwaka huu, tukio litakalofanyikia ukumbi wa Mlimani City ambapo washindi watatu watapatikana.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa shindano hilo, linalofanyika kwa ushirikiano na Mradi wa masuala ya Teknolojia na Ubunifu Bits & Bytes, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin, alisema lengo ni kuwatambua na kuwaendeleza wakulima wanaolima kibunifu.

Alisema, kilimo cha kibunifu kinawanufaisha wakulima kwa kuwa wanapata faida ile ile iliyokusudiwa kwa kuwa kinaokoa mazao na mbegu kupotea wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.

“Tanzania Breweries tumeona nafasi ambayo kilimo inayo katika kuendeleza uchumi wa nchi na hilo linaweza kufanikiwa kwa kutumia teknolojia na ubunifu katika kilimo, hivyo shindano hili linalenga kuwafikia wakulima wengi zaidi”alisema Roberto Jarrin.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa Bits and Bytes Zuweina Farah, alisema katika kuhakikisha kilimo chenye kuhusisha ubunifu na teknolojia unafanikiwa mnamo April 9 watakua SUGECO, na tarehe 10 na 12 watashiriki kwenye kongamano la kilimo biashara mkoani Morogoro.

Aliongeza pia Arusha mnamo April 12 na 13 katika Chuo cha ufundi Arusha kutakuwa na mjadala kuhusiana na kilimo ikiwa pamoja na kutembelea miradi tofauti ya Twende. Huku April 14 hadi 15 itashirikiana na AIESEC kwa Dar na mipango mingine kufanyiwa kazi kufikisha ujumbe kwa wabia tofauti kwenye eneo hili..
Mkurugenzi wa Tasisi Bits and Bytes,Lilian Madeje akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mradi wa ubunifu wa kuinua kilimo nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia nchini(TBL),Roberto Jarrin, akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu udhamini wao wa kuwezesha bunifu za Kilimo
Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa TBL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...