Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.

Ameongeza kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.

“Nawataka wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema Bw.Katemba
 Mkurugenzi wa  Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa  Mashirka Yasiyo ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Mwanza katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mkurugenzi  wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa wadau kutoka katika Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Baadhi ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Mwanza wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...