JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA
WATOTO
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAKWIMU ZA VIFO
VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto inapenda kutoa ufafanuzi wa takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi
nchini. Ufafanuzi huu unatokana na taarifa iliyorushwa na kituo cha Televisioni
cha ITV katika moja ya taarifa zake za habari siku ya tarehe 29 Machi 2018 na
baadaye kuanza kuzunguka katika mitandao ya kijamii inayosema “Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu-UNFPA
limesema idadi ya vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi hapa nchini
imeongezeka hadi kufikia vifo 556 kwa
kila vizazi hai elfu moja (1000) kutokana na changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya afya ikiwamo uhaba wa wauguzi na wakunga”.
Nikiwa Waziri mwenye dhamana ya Afya, napenda
kuufahamisha umma kuwa taarifa hizo sio
sahihi. Na ukweli wake ni kuwa takwimu
za tathimini iliyofanywa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/2016 (Ikiwa ni miaka miwili na nusu iliyopita)
ya Hali ya Afya za Watu Tanzania (TDHS - MIS) ni kuwa vifo vya akinamama
vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila
vizazi hai 100,000 (laki moja) na si vifo 556 kwa kila vizazi hai 1,000 (efu
moja). Aidha nasisitiza kuwa Takwimu
hizi ni za miaka miwili na nusu iliyopita.
Ni
muhimu ikafahamika kuwa Serikali ya awamu ya Tano tangu imeingia madarakani Novemba
2015, imewekeza sana katika sekta ya afya hususani katika eneo la afya ya mama
na mtoto. Tuna imani kuwa endapo
itafanywa Tathmini kama hii iliyofanywa na kusimamiwa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) hakuna shaka kuwa itatuonesha hatua
kubwa tuliyopiga katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Serikali
kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo tumechukuwa hatua mbalimbali zenye
lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Mikakati ambayo serikali ya Awamu ya Tano kwa kushirikiana na
wadau wa sekta ya Afya imewekeza na
kuitekeleza ili kupunguza vifo vitokanavyo
na uzazi ni pamoja na:-
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...