Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema matatizo ambayo yanatokana na uzazi yapo ambayo yanaweza kuzuilika na kuhimiza wadau kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.

Pia ametoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Childbirth Survival International(CSI) ya kuhakikisha wanatoa elimu ya afya salama ya uzazi na kushiriki kwa vitendo katika kufanikisha vifo kwa mama na mtoto vinapungua hapa nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya CSI na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza waanzilishi wa taasisi hiyo Stella Mpanda na Profesa Tausi Kagasheki.

Rais mstaafu Kikwete amesema kumekuwepo na vifo ambavyo vinatokea kwa wajawazito na watoto ambao hawana hatia na kutumia nafasi hiyo kuhimiza wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo hivyo.

Amesema ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu ambayo itasaidia jamii kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa mama mjazito na kubwa zaidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye eneo la afya ya uzazi na vifo. Ameelezea hatua ambazo zinachukuliwa katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya ya taasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda akitoa  historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mafanikio na changamoto wakati wa Maadhimisho ya miaka mitano jijini Dar es Salaam
 Mmoja ya waanzilishi wa Childbirth Survival International(CSI), Profesa Taus Kagasheki akitoa shukrani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake katika kuhakikisha Tanzania tunapunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.
 Mshehereshaji kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI), Babie Kabae akifafanua jambo wakati maadhimisho hayo ambayo yamefanyika jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya waalikwa wakifuatilia hotuba ya rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wakati maadhimisho ya miaka mitano ya ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...