Mkufunzi Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutoka kitengo cha KEIZAN, Janeth Senkondo (akiwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa za ngozi kwenye mafunzo yanayoratibiwa na TanTrade.
Wazalishaji thelathini (30) wa bidhaa za ngozi kutoka Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za
Ngozi Tanzania (TALEPPA) wamejengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ya siku tatu
yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Bw Emmanuel Miselya, Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji
Biashara kutoka TanTrade amesema kuwa lengo la kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa
za ngozi ni kuwasaidia kuwa na ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
‘’Sekta hii ina rasilimali nyingi na ikitumiwa vizuri kwa kushirikiana na wazalishaji wenyewe
Tanzania itakuwa na viwanda vingi vya ngozi na bidhaa zake na wananchi watapata ajira
itakayowaongezea kipato kikubwa kwa sababu kuna fursa kubwa ya masoko ndani na nje ya
nchi hivyo kuongeza wigo wa kodi”, alisema Bw Miselya.
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa TanTrade itahakikisha inatoa mafunzo kwa wazalishaji wa
bidhaa zenye muelekeo wa viwanda ili rasilimali za nchi zitumike vizuri na kuweza kuvutia
ongezeko la uwekezaji nchini.
Nae, Bw Johnson Kiwia, Afisa Viwango kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
amewashauri wazalishaji wa bidhaa za ngozi kuzingatia kutumia malighafi iliyothibitishwa na
taasisi hiyo ili kuwapa ujasiri wa kufanya biashara ndani na nje ya nchi na kuweza kumudu
ushindani wa soko.
Kwa niaba ya wanufaika wa mafunzo hayo, Bw.Timoth Funto, Katibu wa Chama cha
Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA) ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo
wamepata ujuzi wa masoko yatakayowawezesha kutatua changamoto ya namna ya
kusimamia biashara zao ili kukidhi hitaji la msingi lililokuwa linawatatiza katika uzalishaji.
Mafunzo ya awamu ya tatu yamejikita kwenye uzalishaji bora wa bidhaa zenye viwango,
kuzingatia usalama mahala pa kazi na namna ya kubuni bidhaa zenye mvuto na kuendana na
mitindo ya kisasa yenye kupendwa na watumiaji wengi.
Taasisi zilizoshiriki kuwajengea uwezo wazalishaji hao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji kupitia kitengo cha KAIZEN, TBS, VETA, OSHA na DIT kampasi ya Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...