Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Huduma ya Mradi wa mabasi ya mwendo kasi (UDART) imefanya marekebisho katika mfumo wa utoaji huduma hasa katika ukusanyaji wa nauli kutoka kampuni ya Max com Afrika na sasa utafanywa na Shirika la simu la Taifa (TTCL)

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Mawasiliano (UDART) Deus Bagaywa ameeleza baada ya mkataba na Max Com Afrika kuisha baada ya kudumu takribani kwa miaka miwili kuanzia Mei 2016 hadi leo Aprili 14, hivyo wameamua kuwa na mkataba na TTCL kampuni iliyokuwa inawasaidia hapo awali na hii ni kwa lengo la kuboresha huduma zaidi na ukiangalia shirika la TTCL limeboresha sana mitambo yao.

Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wanatoa huduma katika vituo vya mabasi mabadiliko hayo hayatawaathiri, Bugaywa ameeleza wafanyakazi 191waliokuwa wanafanya kazi kupitia Maxcom Afrika na kulipwa na UDART wataendelea na kazi na kubadilishiwa mikataba hivyo hawataathirika.

Aidha ameeleza changamoto zitajitokeza kwa siku mbili hizi ila watajitahidi kutoa huduma kwa ufasaha.

Kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Bugaywa ameeleza kuwa wamejiandaa na mipango ya dharura na wanachukua tahadhari  hivyo wananchi wawe na imani na usafiri huo.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mabadiliko ya utoaji huduma kutoka Maxcom Afrika kwenda kwa Shirika la simu la taifa (TTCL)(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...