*Balozi
wa Wang Ke aongoza Jumuiya ya marafiki wa China ,Tanzania kuwakumbuka
waliopoteza maisha wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SERIKALI
ya Tanzania imeungana na Jamhuri ya Watu wa China katika kumbukumbu ya
vifo vya Wachina 70 waliofarika wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA).
Watanzania
waliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustino Mahiga huku
ikiwakilishwa na Balozi wao nchini, Wang Ke. Kumbukumbu hiyo,
imeandaliwa na Jumuia ya Marafiki wa Tanzania na China ambayo Mwenyekiti
wake Dk.Salim Salim na Katibu wake ni Joseph Kahama.
Kabla
ya kuweka mashada kwenye makaburi kwenye makaburi ya wachina hao ambao
wengi wao ni wataalamu na wahandisi katika ujenzi wa reli, ilitolewa
historia fupi ya vifo vyao.
Akizungumza
baada ya kuweka mashada, Balozi Mahiga alisema ujenzi wa reli hiyo
ulithibitisha urafiki wa kutoka moyoni kati ya nchi hizo mbili na
kufafanua ujenzi wake ulifungua milango kwa China kujenga viwanda
vingine kama UFI na Kiwanda cha Nguo cha Urafiki."Wakati
wa ujenzi huu damu zilimwagika, wachina wamepoteza maisha na wengine
wamebaki na ulemavu wa kudumu...hivyo urafiki wetu sisi na China ni wa
damu," amesema.
Naye,
Balozi Wang amesema nusu ya karne iliyopita, kupitia ombi la Rais wa
Tanzania, Julius Nyerere na Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda, viongozi wa
kizazi cha China, Mwenyekiti Mao Zedong na Waziri Mkuu, Zhou Enlai
walifanya maamuzi ya kimkakati na kihistoria kusaidia ujenzi wa TAZARA.
Mnara
wa Makaburi ya Wachina waliokuwa wakijenga Reli ya Tazara ambao
walifariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo miaka zaidi ya 40 iliyopita.Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Agustine Mahiga akitoa heshima na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, kwenye Mnara wa makaburi ya Wachina waliofkuja kutengeneza Reli ya Tazara
Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Agustine Mahiga akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakiongoza kuweka mashada ya maua kwenye moja ya kaburi la wakandarasi waliofika nchini kujenga reli ya Tazara
Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Agustine Mahiga akihutubia Viongozi na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika sherehe ya kitamaduni ya watu wa china ya kuwakumbuka mafundi waliojenga reli ya Tazara.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, akihutubia na kutoa historia fupi ya ushirikiano wa Tanzania na China ulivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...