Na
Lusungu Helela-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa yeyote atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye misitu atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza jana wilayani Kishapu wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani humo, Mkuu wa Mkoa alipiga marufuku kukata miti bila ruhusa yake au ya Mkuu wa wilaya.
Telak alisema marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia katika Wilaya hiyo inatisha hakuna mahindi yanayostawi kutokana na kutokuwa na mvua ya kutosha.
‘’Mtu yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake ni lazima aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali ajue jela inamwita.
Wakati huo huo, Telak alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanawakamata wale wote watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu hoja zilizotolewa na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa Misitu jana wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Anna Matinye akichangia hoja jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akiwasilisha maada kwa wadau mbalimbali wa uhifadhi wa Misitu kwa kuwasomea baadhi ya vipengele kwenye kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu jana wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...