*Mwili wahifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma,DC Kongwa azungumzia mazingira ya ajali

Na Ripota, Dodoma

INASIKITISHA na inaumiza sana!Hii ndio kauli unayoweza kuielezea kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Izengo Ngussa.

Kifo cha Ngussa kimetokana na ajali ya gari yake kugongana na lori la mafuta eneo la Mbande Makaravati wilayani humo mkoani Dodoma.

Kutokana na gari yake kuharibika vibaya na kulaliwa na roli imesababisha mwili kubebwa na kipande cha gari lake kwa ajili ya kwenda kutolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), kwani uling'ang'ania kwenye bodi.Tukio la ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Ngussa limetokea usiku wa leo.Alikuwa kwenye gari ndogo akitokea Dodoma Mjini.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Michuzi blog kuwa gari ya Mkurugenzi yenye namba T 619 DMA baada ajali hiyo gari yake ilikandamizwa na roli la mafuta.Hali hiyo ilisababisha mwili wake kuungana na bodi la gari lake na kushindwa kutolewa katika eneo la tukio.Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kimedai tangu jana asubuhi shughuli za utoaji mwili huo zilianza.Hata hivyo hazikufanikiwa kwani mwili wake ulikuwa umeng’ang’ania katika bodi ya gari.
"Saa 8 mchana kipande cha gari kilichukuliwa na gari la jeshi na kisha kupelekwa Temesa Dodoma ili bodi la gari litanuliwe na kuutoa mwili," kimedai chanzo hicho.Kwa sasa mwili umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa Dodoma, baada ya Temesa kufanikiwa kuutoa mwili kwenye gari saa 10 ya jioni.

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi amezungumzia kutokea kwa ajali hiyo na kuthibitisha kifo cha Mkurugenzi huyo.Amefafanu ajali imetokea  usiku na taarifa zikaanza kuzagaa alfajiri na kwamba alikuwa anatokea njia ya Dodoma mjini kuelekea Kongwa.

"Kutokana na mazingira ya ajali tulipata  wakati mgumu tulipokuwa tunautoa mwili kwenye gari take," ameongeza.Ameelezea kazi iliyofanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na Kikosi cha Zimamoto ambao wameshiriki kikamilifu katika ukoaji. Ndejembi amefafanua  taarifa rasmi itatolewa na Jeshi la Polisi ambalo linaendelea kufanya uchunguzi.
Akimzungumzia Mkurugenzi Ngussa, amesema wamempoteza mtumishi mwadilifu na aliyekuwa anaipenda kazi na kwamba amefanya naye kwa miaka miwili."Amesaidia  wilaya kupata hati safi katika ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)," amesema.

Kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dk.Caroline Damian amethibitisha kupokea na kuuhifadhi mwili wa Mkurugenzi huyo."Mwili wake umeumia sana katika maeneo ya kichwani.Amevunjika mkono na mguu mmoja wa kushoto," amesema.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, White Zuberi amesema Wilaya hiyo imepata pigo kutokana na kifo cha Mkurugenzi huyo  aliyekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...