Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa Wakulima wa pamba kuhusu Mizani sahihi zinazotakiwa kutumika wakati wa msimu wa ununuzi wa pamba, elimu hii ya vipimo ni ya muhimu kwa Wakulima wakiwa katika maandalizi ya kuelekea katika msimu wa ununuzi wa pamba . 

Mpaka sasa Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora imetoa elimu kwa Wakulima wa pamba katika wilaya mbili (2) ambazo ni Nzega na Igunga, na takribani kata 20 zimefikiwa na kupata elimu hiyo ambapo zoezi bado linaendelea. 

Wakulima wa pamba wameipokea kwa furaha elimu ya utambuzi wa mizani sahihi iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo, kwani itawasaidia kuwabaini kwa urahisi wale wanaotumia mizani ambazo hazija hakikiwa wakiwa na lengo la kutaka kuwaibia pamba yao. 

Pia, elimu ya utambuzi wa mizani sahihi zilizohakikiwa na WMA itawasaidia Wakulima kuuza pamba safi, kwani apo awali walikuwa wanajihusisha na uchafuzi wa pamba kwa kuweka michanga, kokoto, mafuta ya kenge pamoja na maji ili waweze kuongeza uzito katika pamba pindi waendapo kuiuza.

Wakala wa Vipimo inatoa wito kwa wadau wote wa zao la pamba kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yeyote haswa uchakachuaji wa mizani wakati wa ununuzi wa pamba, kwani kwa yeyote atakaye kamatwa kwa makosa hayo atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura na. 340.

Pia, WMA ina namba maalumu kwa ajili ya wananchi kupiga na kupata msaada pindi wakutanapo na changamoto za kivipimo, namba hiyo ni 0800 110097 namba hii ni bure kabisa.
 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakioneshwa sehemu ya kuweka lakili (seal) na kubandika stika ya WMA mara baada ya mizani kuhakikiwa.
 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakielekezwa na afisa vipimo namna ya kutambua mizani ya saa (salter) iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo.
Afisa Vipimo akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyo hakikiwa kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Igunga kijiji cha mwabakina kata ya mbutu mkoani Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...