Mwenyekiti wa Jumuiya ya Muzdalifa Maalim Abdalla Hadhar akitoa Elimu kwa Wanafunzi na Watoto mayatima baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Maziwa Cha Bakhresa Fumba kwa ziara maalum ya kimasomo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima itakayofika kilele chake ttarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
Msimamizi wa mashine za kiwanda cha Maziwa cha Bakhresa Salum Khamis Faki akifafanua baadhi ya maswali yaliouliulizwa katika ziara ya kimasomo ya Wanafunzi na Watoto mayatima wa Skuli ya Alfarouk Aktas iliopo Shakani Magharibi B ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima itakayofika kilele chake tarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
Wanafunzi na Watoto mayatima pamoja na Walimu wao wa Skuli ya Al Farouk Aktas wakiangalia Utengenezaji na Uwekaji maziwa katika Chupa na Vifuko maalum katika ziara ya kimasomo Kiwanda cha Maziwa cha Bakhresa Fumba ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima itakayofika kilele chake tarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
Mfanyakazi wa Kitengo cha Uzalishaji Maziwa wa Kiwanda cha Bakhresa Fumba Mshindo Yussuf akigawa Maziwa kwa Wanafunzi na Watoto Mayatima waliotembelea Kiwandani hapo kwa ziara ya kimasomo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima itakayofika kilele chake tarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
Watoto mayatima wa Skuli ya Alfarouk Aktas na Walimu wao wakifanya mazoezi ya matayarisho ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima ambayo itafika kilele chake tarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
Wanafunzi na Watoto mayatima wa Skuli ya AL Farouk Aktas iliopo Shakani Magharibi B pamoja na Walimu Wao wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Maziwa Cha Bakhresa Fumba kwa ziara maalum ya kimasomo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima itakayofika kilele chake tarehe 8, April 2018 Fumba Magharibi B Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...