Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta pamoja na Mkurugenzi wa Masoko
Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, wakikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la madarasa kwa ajili ya
wanafunzi wenye uhitaji maalum katika Shule ya Msingi Msasani, Dar es
Salaam, Aprili 6, 2018. Msada huo ni ya sehemu ya Benki ya CRDB katika
kuisaidia jamii. Ambapo Benki hiyo imejiwekea sera maalum ya kusaidia
jamii ambayo inalenga kurudisha kiasi cha asilimia moja ya faida ya
Benki hiyo kila mwaka, ili ziende katika shughuli za kijamii, hususani
katika nyanja za elimu, afya na mazingira.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza na kutoa pongezi
kwa Benki ya CRDB ambapo aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo wa
madarasa na madawati kwa shule ya
msingi Msasani. katikati ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa
Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na kulia ni Mwalimu
Edward Molel.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta na Mkurugenzi wa Masoko
Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, pamoja na
wanafunzi wenye uhitaji maalum, wakimsikiliza mmoja wanalimu wa shule
hiyo alipokuwa akieleza jambo kwa lugha ya alama.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akimshukuru Mkurugenzi wa Masoko
Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa kwa msaada huo waliotoa.
Picha ua pamoja na baadhi ya wanafunzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...