Programu ya Football for Friendship (F4F) 2018 inabadilisha ndoto ya kombe la Dunia la FIFA kuwa kweli kwa Zipora Mollel pamoja na Laigwanani Lomayani Mollel, vijana hao kutoka kabila la Maasai wamechaguliwa kwenda Russia kuiwakilisha Tanzania huku gharama zote zikibebwa na F4F. 

F4F ni programu ya kimataifa ya watoto ya kila mwaka inayoratibiwa na kampuni ya kimataifa Gazprom ambayo inaunga mkono miradi ya kijamii ulimwenguni na kuweka viwango vipya kuhusiana na sera za kijamii.

Inatarajiwa kufanyika Moscow, Russia kuanzia Juni 8-15, kuelekea michuano ya Kombe la Dunia, lengo la programu hii ni kutangaza maadili yanayohusiana na mpira wa miguu kwa vijana wadogo ikiwa ni pamoja na kuheshimu mila, utaifa na usawa.

Laigwanani Mollel ataiwakilisha Tanzania akiwa mchezaji anayechipukia wakati Ziporah Mollel yeye atashiriki kama mwanahabari chipukizi, watakuwa wawakilishi wa nchi kwenye kombe la Dunia licha kwamba timu ya taifa imeshindwa kufuzu katika mashindano hayo. Wataungana na wachezaji wenye umri wa miaka 12 pamoja na waandishi kutoka mataifa 210 na kujumuika kushiriki programu ya siku nane (8).

Mwaka 2018 mataifa mapya 147 na kanda zitashiriki programu ya F4F inayohusisha watu 3,700 wenye umri kati ya miaka 12 na 16 walioshiriki program hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.

Laigwanani Mollel na Ziporah (miaka 12) wataambana na meneja wa uendeshaji kutoka Lengo Football Academy, Bw. Amani Mzava, kocha Bw. Alvin Girelisu. Lengo Football Academy inajivunia kushirikiana na Clouds FM na Clouds TV. Mwanahabari mashuhuri wa michezo Shaffih Dauda kutoka Clouds FM/TV ataongozana na msafara wa watanzania kwenda Russia kuiwakilisha Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...