Na Elisa Shunda, Bagamoyo
JUMUIYA ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani imeadhimisha siku ya wazazi kwa mkoa huo kwa kuchangia kutoa damu chupa 120 na kutoa mifuko 50 ya simenti,mabati 100 na matofali 200 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu na Laki Saba na Hamsini kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Amani Voda iliyopo Mbwewe wilayani Bagamoyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa na wilaya waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamesema kuwa jukumu kubwa walilonalo jumuiya ya wazazi ni kuhakikisha wanajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanatumia nguvu na mali kusaidia katika elimu,mazingira na afya ambayo yanagusa jamii ya watu wengi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno alisema kuwa muda haumsubiri mtu na kuwasisitiza wawakilishi wa majimbo na kata wa chama hicho kutekeleza ahadi walizoahidi kuzitoa kwa wananchi wao wahakikishe wanazitekeleza wao kama viongozi hawatakubali chama kije kiadhibiwe katika chaguzi zijazo kwa ajili ya uzembe wa mwakilishi wa wananchi hao.
“ndugu zangu wawakilishi mliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha bungeni na kwenye vikao vya halmashauri ni muda muafaka sasa wa kuhakikisha kabla ya uchaguzi mkuu haujafika hakikisheni mnatatua changamoto na kero za wananchi wenu mnaowawakilisha,haiwezekani chama chetu kiadhibiwe na wananchi ambao ndiyo wapiga kura kwa uzembe wa kutowajibika ipasavyo kwa watu hawa waliokuchagua hata nyie wenyeviti wa serikali za mitaa wahudumieni kwa haki wananchi wenu kama inavyotakiwa bila ya upendeleo” Alisema Maneno.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani, Gama J Gama na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda wakipanda miti katika eneo la Kituo cha Afya cha Lugoba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...