TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa kujihami Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika Mei mwaka huu.

Rais wa Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki, Kennedy Said alisema jana kuwa maandalizi ya mashindano hayo yameanza.

Alisema mashindano hayo yatakutanisha wachezaji zaidi ya 70 kutoka nchi za Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda na wenyeji Tanzania.

Kennedy ambaye pia ni Rais wa Tae Kwo-ndo Tanzania alisema zimealikwa nchi za Ethiopia na Sweden kushiriki mashindano hayo na zawadi mbalimbali zimeandaliwa kwa ajili ya washindi.

Kennedy alisema Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindani hayo kutokana na mkutano wa nchi saba wanachama uliofanyika Kampala,Uganda Desemba mwaka jana.

Alisema washindi wa mashindano hayo watapata nafasi ya kushiriki fainali ya kuwania ubingwa wa mchezo huo Afrika utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Agosti mwaka huu.
Wachezaji wa Tae kwo-ndo wakijiandaa kwa mazoezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...