NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...