Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MWANADIPLOMASIA wa siku nyingi nchini, Balozi Juma Mwapachu ameshauri mfumo wa elimu uliopo nchini ufanyiwe mabadiliko ikiwemo kuongeza vyuo vya ufundishaji walimu  kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu kinachotolewa nchini.

Balozi Mwapachu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha pili kiitwacho ‘ Tanzania in the Age Of Change And Transformation’ na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wastaafu, waadhiri, majaji wastaafu, wanadiplomasia na wasomi kada mbalimbali.

Balozi Mwapachu amesema pamoja na juhudi  zinazoendelea kufanywa na Serikali kuboresha elimu nchini, bado kuna changamoto nyingi  katika elimu hiyo ambayo kwa kiasi fulani inakwamisha mipango mizuri ya baadae.

“Hakuna ubishi kuwa elimu ndiyo msingi  kwa Taifa lolote, hivyo ili kupiga hatua ipo haja ya kutafuta mapinduzi katika elimu yetu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu…hili zaidi ni kwa kuangalia mfumo wa ufundishaji wa vyuo vya kufundishia walimu,"amefafanua  Balozi Mwapachu.

Amesema uwepo wa idadi ndogo ya vyuo vinavyozalisha walimu hao ni sababu kubwa inayochangia kushuka kwa kiwango hicho cha elimu kinachotolewa nchini  katika ngazi zote kuanzia elimu ya awali hadi  chuo kikuu, jambo alilosema kuwa  ni vyema likafanyiwa mabadiliko mapema ili kuzalisha wanafunzi wenye tija.

Aidha katika hatua nyingine Balozi Mwapachu alizungumzia sekta binafsi kwa kusema kuwa pamoja na muendelezo mzuri unaofanywa na Serikali hususani katika uendelezaji wa kilimo,kuna haja ya kuongezwa kwa jitihada ili kuwaa na tija zaidi. 

“Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kulipa msukumo suala la uendelezaji kilimo na viwanda, na zaidi kwa namna ambavyo Serikali ilivyowekeza katika mapinduzi ya viwanda kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ifikapo Mwaka 2020,” amesema Balozi Mwapachu.

Pia amesema bado hali siyo nzuri kwa mahusiano ya wafanyabiashara na Serikali kutokana na kutokuwepo kwa mahusiano mazuri siku za nyuma, tofauti na sasa ambapo mabadiliko yameanza kuonekana.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho Profesa Mark Mwandosya, mbali na kumpongeza Mwapachu kwa kuzindua kitabu hicho, alisema  kuna umuhimu wa watanzania kuwa na utamaduni wa kuandika vitabu katika masuala mbalimbali kwa kuwa vinabeba kumbukumbu ya miaka mingi.

Amesema kila kitu kina misingi yake, na kwamba hakuna kinachoweza kusahaulika kirahisi kama vitabu, bila kujali kuwa maandiko hayo ni mazuri au mabaya kwa kuwa maandiko mabaya hupata fursa ya kuboreshwa.
 Balozi Juma Mwapachu akiwa na mkewe Rose Mwapachu wakiwa wameshika kitabu kinachofahamika Tanzania in the Age Of Change and Transformation jana jijini Dar es Salaam baada ya kukizindua.Wengine wanaoshuhudia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi(kulia) na upande wa kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo Profesa Mark Mwandosya akiwa na mkewe.
Mgeni rasmi Profesa Mark Mwandosya akizindua kitabu cha Tanzania in the Age Of Change and Transformation jana Dar es Salaam ambacho mtunzi wake ni Balozi Juma Mwapachu. Aliyeshika kitabu hicho ni qmkewe Balozi Mwapachu, Rose Mwapachu wakati kutoka kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi na Balozi Juma Mwapachu
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu hicho Prof.  Mark Mwandosya akichukua kitabu kabla kukizindua rasmi.Wanaoshuhudia ni Balozi Juma Mwapachu na mkewe Rose Mwapachu pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi .
 Mgeni rasmi Prof. Mark Mwandosya akichukua kitabu kabla kukizindua rasmi.Wanaoshuhudia ni Balozi Juma Mwapachu na mkewe Rose Mwapachu pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi .
 Balozi Juma Mwapachu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha  Tanzania in the Age of Change and Transformation jijini Dar es Salaam
Mgeni Profesa Mark Mwandosya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jana jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...