Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta (hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuvikwa cheo cha Brigedia Jenerali iliyofanyika siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington, DC.Balozi Wilson Masilingi alimwagia sifa kwa kazi nzuri anayofanya kwa nidhamu ya hali ya juu, kujituma kwake na kushirikiana ndio chachu ya mafanikio yake.
Wambata wengine waliovikwa vyeo vya Brigedia Jenerali ni Brig Gen AS Nwamy- Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brig Gen AM Alphonce Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brig Gen JJ Mwaseba- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Brig Gen RC Ng'umbi- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akitoa hotuba fupi ya kumpongeza Brigedia Jenerali Adolph Mutta kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akiondoa cheo cha Colonel na kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbu wa mkutano a Nyerere hall uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimvua kofia ya cheo cha Colonel na kumvisha kofia ya cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa Nyerere Hall.uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...