Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

CHAMA Cha Kijamii (CCK) kimekutana na wawakilishi kutoka mikoa 20 nchini kwa mara ya kwanza tangu kilipopata usajili wa kudumu mnamo mwaka 2012.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam  katika mkutano huo aliyekuwa mwenyekiti ambaye amejiuzulu nafasi yake Costastine Akitanda ameeleza kutokana na majukumu mengine aliyopewa ya kusimamia kilimo barani Afrika ameona aachie nafasi hiyo na anaamini Chama hicho kitafika mbali zaidi.

Akitanda ameeleza lengo la chama hicho ni kuwasaidia wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii hasa uchumi na kufafanua wanachama ndio wenye maamuzi katika chama katika kuhakikisha chama kinaenda mbele zaidi.

Kuhusu suala la ruzuku kwa vyama vya siasa Akitanda ameshauri kuwa ruzuku zitolewe kugharamia chaguzi ili kuwe na usawa katika uwakilishi na si kutolewa katika vyama.

Katibu wa chama hicho Renatus Muhabi ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizopo kama vyama vingine kama vile kukosa ruzuku  jambo linalosababisha  ugumu katika kuendesha chama na amewaomba wanachama kuendeleza malengo ya chama hicho sambamba na kushika dola mwaka 2020.

Hivyo amewataka wasikatishwe tamaa na upotoshaji kuhusu hali ya kisiasa ya sasa kuhusu utendaji kazi wa awamu ya tano inayofanya mapinduzi katika jamii ya kitanzania.

Aidha amesema kuwa chama hiki kimepokelewa vizuri na wananchi hivyo wanataraji watafanya mapinduzi katika siasa na kuifikisha nchi katika mahali sahihi.

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo ameshiriki mkutano huo na ameeleza kuwa amefurahi kualikwa na chama hicho ili aweze kutoa nasaha na ameeleza kuwa vyama vya siasa lazima viwe na urafiki kwa kuzungumza pamoja.

Amefafanua hiyo italeta siasa za amani na kusikilizana na hakuna chama pinzani bali vyote vina mlengo wa kuleta maendeleo nchini. Kuhusu ruzuku kwa vyama ameeleza ni muhimu zitolewe katika chaguzi ili kuweza kupata uwakilishi bungeni.

Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama ya siasa kama vile UPDP, SAUTI YA UMMA, TLP na Demokrasia Makini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...