*Watakaofanya udanganyifu wa aina yoyote kukiona cha moto
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
BARAZA
la Mitihani la Tanzania(Necta) limetoa onyo kali kwa wamiliki wa
shule,walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa
mitihani ya Kidato cha Sita na Kozi za ualimu inayoanza kesho Mei 7 hadi
Mei 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa baraza hilo ni kwamba jumla ya
watahiniwa 87,643 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo
kati yao watahiniwa wa shule ni 77,222 na watahiniwa wa kujitegemea ni
10,421.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa
Necta Dk.Charles Msonde ametangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo
ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.Akisisitiza
Dk.Msonde amesema baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua yeyote
atakayejihusisha kufanya udanganyifu katika mihitani kwa mujibu wa
kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi.
Amefafanua ikiwa
panoja na kuwafutia matokeo yote watahiniwa watakaobainika kujihusisha
na vitendo vya udanganyifu."Wadadau wore wanaombwa kutoa taarifa katika
vyombo husika kila wanapobaini uwepo wa mtu au kikundi cha watu
kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile," amesema
Dk.Msonde.Pia amesema baraza linatoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano
katika kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa amani na utulivu .
"Wananchi
wanaombwa kuheshimu eneo la mitihani na kuhakikisha asiyehusika
haingii maeneo ya shule,"amesema Dk.Msonde.Ameongeza wamiliki wa shule
na vyuo wanatakiwa kutambua shule na vituo vya maalum vya mitihani na
hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingiliwa majukumu ya usimamizi wa
mitihani kwa kipindi chote hicho.
" Baraza halitosita kukifuta
kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake
ubahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa,"amesema Dk.Msonde.Ametumia
nafasi hiyo kutoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri
kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taiga zinazingatiwa
ipasavyo.
Kwa upande wa wawatahiniwa ,amesema baraza linaamini
walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha elimu ya sekondari na
kozi za mafunzo ya ualimu.Hivyo matarajio yao watahiniwa watafanya
mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshwe
uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi walioupata kipindi cha
mafunzo yao.
Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo alipokuwa akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...