Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
MWENYEKITI wa Baraza la Wafanyakazi wa Tasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dk.Kassim Nihuka amesema pamoja na mafanikio ambayo imeyapata taasisi hiyo bado wangepata mafaniko makubwa zaidi iwapo changamoto zinazowakabili ikiwamo ya uhaba wa watumishi pamoja na miundombinu ingekuwa imepata ufumbuzi wake huku akifafanua tayari wameweka mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto hizo.
Dk. Nihuka ametoa kauli wakati anazungumza kwenye Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima uliofanyika leo ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando.
Akizungumza kwenye hotuba yake kwa mgeni rasmi ,Dk.Nihuka amesema mafanikio hayo huenda yangekuwa makubwa na mengi zaidi kama siyo changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwamo za ukosefu wa ofisi za kudumu katika baadhi ya mikoa, upungufu wa wafanyakazi kutokana na kustaafu na vifo pamoja na
upungufu wa fedha za ndani.
Pia amesema ili kuendana na na msimamo wa Serikali wa Awamu ya Tano ,Menejimenti ya taasisi hiyo imedhamiria kuimarisha ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha yanaenaelekezwa katika kutekeleza malengo ya kipaumbele kadiri ya mpango kazi wa taasisi na ule wa vituo,kampasi,idara na vitengo kwa ujumla.
"Katika kutekeleza hili wakufunzi wakazi, wakuu wa kampasi na mkuu wa idara ya mafunzo yanaagizwa kusimamia ukusanyaji wa ada kwa umakini mkubwa pamoja na kuhakikisha wanafunzi wale tu waliolipa ada ndio wanasajiliwa na kupata huduma katika vituo vyote,"amesema Dk.Nihuka.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dk.Kassimu Nihuka akizungumza kuhusu mafanikio na changamoto mbele ya wajumbe wa baraza hilo waliokutana leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akizungumza leo wakati akifungua rasmi Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wakishiriki mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...