*Asema anatambua juhudi zake na mchango wake, 
pia ametambua umri wake
*Kinana ashukuru kukubaliwa na Rais, aeleza 
Mangulla alivyojitoa mhanga
ugumu wanaupata

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Rais Dk.John Magufuli amesema ametafakari kwa kina na kuamua kuridhia kung'atuka kwa Katibu Mkuu  wa Chama hicho Abdulrhaman Kinana lakini hadi atakapomaliza muda wake ndipo atapumzika.

Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na Wajumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema anatambua juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Katibu MKuu wao.

"Ni zaidi ya mara mbili Katibu Mkuu wetu ameomba kumpuzika lakini nikawa namkatalia na hata alipokuwa anaanzisha hoja hiyo kisiri siri mimi nilikuwa naanzisha pointi nyingine.

"Lakini nieleze tu natambua juhudi kubwa ambazo amefanya.Lakini pia nikatambua kuna makatibu wakuu wengi wamekitumikia chama chetu na wengi tu maana walikuwepo hata kabla mimi kuanza shule ya msingi.

"Natambua umri alionao Katibu Mkuu wetu.Hivyo  nilimuita mzee Shein(Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) nikamueleza akaniambia mruhusu akapumzike,nikamuita mzee Mkapa naye mkubalie.Hivyo nimekubalia acha akampumzike,"amesema.

Pia amesema jana alimuita Katibu Mkuu Kinana na wakazungumza akimini huenda atabadili mawazo yake lakini bado akabaki na mawazo."Hivyo nimemkubalia akapimzike lakini atapumzika baada ya kumaliza muda wake,"amefafanua Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Magufuli.

KINANA ASHUKURU KUKUBALIWA KUPUMZIKA

Wakati huo huo Katibu Mkuu Kinana  amesema kuna wakati wa kufanya kazi na wakati wa kupumzika na anaelewa ugumu ambao CCM wanaupata wa kutomkubalia.

"Naangalia nyuso zenu zinaonesha namna ambavyo hampo tayari kunikubalia lakini Mwenyekiti wetu amesema tumewahi kuwa na makatibu wakuu wengi na kweli tumekuwa na makatibu wakuu saba kabla yangu. Hivyo nakushukuru Mwenyekiti kwa kunikubalia, nashukuru Makamu Mwenyekiti  kwa kunikubalia na  nashukuru mzee Mangula kwa kunikubalia.

"Nakumbua kuna siku Mwenyekiti alikuja pale Lumumba na uliamua kujitoa mhanga kwani alipokuuliza kuhusu kupumzika ulimwambia anikubalie.Mwenyekiti kama alikukasirikia hivi lakini nashukuru sana maana ulinisaidia na ulijitoa mhanga,"amesema Kinana.


Amesema amekitumikia Chama hicho kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 30 lakini kwa kipind cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013 alijitolea sana ndani ya CCM lakini hatimaye anashukuru kwa kukubaliwa kwa ombi lake na Mwenyekiti wao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) ya kumuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  akisema machache ya kushukuru baada ya  barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli  na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018

 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  akisema machache ya kushukuru baada ya  kuwasilisha barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli  na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli,  baada ya kumkubalia, akimshukuru na kumwombea kila la heri Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  baada ya kusoma barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...